Jumatano, Septemba 13, 2017

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Namera Group of Industries Bw. Hamza Rafiq Pardesi   ambaye ameahidi kununua pamba yote itakayozalishwa nchini kuanzia msimu ujao.(L) Ni Meneja wa Namera Bwana Muhammad Waseem. Waziri Mkuu amekutana nao leo Septemba 12/ 2017 Ofisini kwake Dar es salaam. 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Namera Group of Industries Bw. Hamza Rafiq Pardesi ameahidi kununua pamba yote itakayozalishwa nchini kuanzia msimu ujao. Waziri Mkuu amekutana naye leo Septemba 12/ 2017 Ofisini kwake Dar es Salaam
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Kwanza mkurugenzi huyo Aahidi kununua pamba yote itakayozalishwa nchini

 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Namera Group of Industries Bw. Hamza Rafiq Pardesi ambaye ameahidi kununua pamba yote itakayozalishwa nchini kuanzia msimu ujao.



Amekutana na Bw. Pardesi  (Jumanne, Septemba 12, 2017)  kwenye makazi ya Waziri Mkuu Oysterbay jijini Dar es Salaam na amesema kwamba tayari Serikali imeanza kuwahamasisha wakulima kuongeza uzalishaji kwa kuwa kuna soko la uhakika.


Waziri Mkuu amempongeza Bw. Pardesi kwa kuiunga mkono Serikali katika mpango wake wa kukuza uchumi kupitia sekta ya viwanda. Kampuni ya Namera Group of Industries inamiliki kiwanda cha nguo cha NIDA na cha Namera vya jijini Dar es Salaam.Kampuni inatarajia kufungua kiwanda kingine cha nguo wilayani Kahama.

Pia Waziri Mkuu amesema katika kuhakikisha zao la pamba linapewa kipaumbe alikutana na wakuu wa mikoa yote inayolima pamba Ijumaa, Septemba 8, 2017 na aliwaagiza wasimamie zao hilo kwa karibu ili kuinua uzalishaji wake na kuwaongezea kipato wananchi hususan wakulima wa zao la pamba.

Amesema Serikali imeamua kufufua mazao makuu matano ya biashara ambayo ni pamba, chai, kahawa, korosho na tumbaku ili kuwawezesha wakulima kupata tija na kuondokana na umasikini wa kipato, hivyo kukuza uchumi wa Taifa.

Waziri Mkuu amesema Serikali imeamua kusimamia kilimo cha pamba kuanzia maandalizi ya shamba, kupanda, matumizi ya pembejeo na dawa, kuvuna na kutafuta masoko, hivyo ahadi yao ya kununua pamba yote ni faraja kwa wakulima.

“Nimefurahishwa na uamuzi wenu wa kutaka kununua pamba yote itakayozalishwa nchini kuanzia msimu ujao kwani kwetu sisi ni faraja kwa sababu wakulima walipunguza uzalishaji baada ya kukosa soko la uhakika.”

Kwa upande wake Bw. Pardesi amemuhakikishia Waziri Mkuu kwamba kampuni yao inauwezo wa kununua pamba yote inayozalishwa nchini na kuichakata katika viwanda vyao na kutengeneza nguo zitakazouzwa nchini kwa bei nafuu.

Amesema kwa sasa wameajiri mafundi katika viwanda vyao ambao watakuwa wa nashona nguo na kuziuza nchini kwa gharama nafuu ili kuwawezesha wananchi wa hali ya chini kumudu kununua na kuondokana matumizi ya nguo za mitumba.

“Mheshimiwa Waziri Mkuu sisi Namera tuko tayari kununua pamba yote inayozalishwa nchini kwani viwanda vyetu vinafanya kazi ya kuchambua pamba, kutengeneza nyuzi na majora kisha tunashona nguo na kuziuza. Hapa Kazi Tu maana bila ya kufanya kazi huwezi kuheshimika.”

Hata hivyo Mkurugenzi huyo amesema kitendo cha kununua pamba inayolimwa nchini na kuchakata katika viwanda vyao kwa lengo la kutengeneza nguo za aina mbalimbali wataiwezesha Serikali kuokoa fedha nyingi za kigeni zilizokuwa zinatumika kuagiza nguo nje ya nchi.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU, 
JUMANNE, SEPTEMBA 12, 2017.

NDUNGAI AWATAKA WAPINZANI WAJIPANGE,AWACHIMBA MKWARA.


SPIKA wa Bunge, Job Ndugai, amepiga mkwara wabunge wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuwa wanapotaka kupambana naye lazima wajipange na wasimchukulie kirahisi rahisi kwa kuwa hawatammudu.

Ndugai aliyasema hayo bungeni jana baada ya kipindi cha Maswali na Majibu alipokuwa akitoa matangazo mbalimbali kama ilivyo ada.

Alifikia hatua hiyo alipokuwa akijibu shutuma zilizotolewa juzi na Mbunge wa Malindi (CUF), Ali Saleh, kuhusu uamuzi wa Naibu Spika wa kutangaza safu mpya ya viongozi wa CUF wakati kuna uongozi mwingine.

“Mheshimiwa Ali Saleh alisema jana (juzi) hapa ingawa sikuwapo na leo kwenye taarifa ya upinzani amerudia rudia tena kwenye utangulizi maneno yale yale.

Sasa hawa rafiki zangu wanapenda sana kunituhumu, lakini nawaambia kila mtu mumsome vizuri mmwelewe… Am a smart  person (niko makini), hivyo mnapokuja kwangu mjipange kidogo msifikiri ufupi huu ni shida,” alisema Ndugai.

Juzi bungeni, Ali Saleh alimhoji Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson, kuwa iweje atangaze safu mpya ya uongozi ilhali bado kuna uongozi halali wa chama hicho ndani ya Bunge hilo.

Saleh alisema wabunge wa chama hicho wameshafanya mabadiliko ya uongozi baada ya wabunge wengine kuondolewa bungeni, hivyo kauli ya Naibu Spika kwamba kuna safu nyingine mpya imewashangaza.

“Mheshimiwa Naibu Spika inakuwaje unatangaza kuwa kuna viongozi wapya wakati hakuna sehemu iliyoelezwa kuwa uongozi uliokuwepo umebatilishwa? Sisi tumeshafanya uchaguzi wetu humu na tayari tuna viongozi?“ alihoji Saleh.

Jana, Ndugai alisema kazi yake ni kutangaza na ataendelea kutoa matangazo mbalimbali yanayoletewa na vyama vya siasa kwa kuwa ndiyo kazi yake.

Alisema hahusiki na vikao vya vyama vya siasa, hivyo anapotangaza mabadiliko haoni sababu yoyote ya kubebeshwa lawama na badala yake wajiangalie.

“Mimi leo hii Mbowe akiniletea mabadiliko kuwa amembadili Waziri Kivuli natangaza. Kazi yangu ni kutangaza, maana mnapokaa huko kwenye vikao vyenu mimi si mmoja wa wajumbe. Sasa mnapolalamika kuwa nimefanya maamuzi (uamuzi), maamuzi (uamuzi) yapi au nimeridhia wapi,” alihoji Ndugai.

Juzi, Dk. Tulia aliwatangazia wabunge kuwa Chama cha Wananchi (CUF), kimepata uongozi mpya  hali iliyosababisha baadhi ya wabunge kuanza kuhoji uhalali wa uongozi huo mpya.

Kwenye uongozi huo mpya, Mwenyekiti ni Maftah Nachuma, Mbunge wa Mtwara Mjini na Katibu wake ni Rukia Kassim Ahmed wakati Mnadhimu atakuwa Maulid Mtulia ambaye ni Mbunge wa (CUF) Kinondoni na Mweka Hazina ni Sonia Magogo.

Dk. Tulia aliwatangazia wabunge kuwa Bunge limepokea barua ya Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bara, Magdalena Sakaya, kuliarifu kuwa wamepata uongozi mpya.

“Waheshimiwa wabunge kwa kawaida bungeni kunakuwa na Kambi Rasmi ya Upinzani lakini vyama navyo huwa vina uongozi wao, hivyo CUF wametuletea safu mpya ya uongozi,” alisema Dk. Tulia.

Wanawake wenye ulemavu wa ngozi kuandika historia mpya kwa kupanda mlima Kilimanjaro.   Mwanaharakati wa haki za binadamu na mp...