Jumatano, Januari 10, 2018

Yanga Leo kukipiga na URA




KIKOSI cha Yanga, leo kitapambana na URA ya Uganda katika mchezo wa nusu fainali ya michuano ya Mapinduzi inayoendelea kutimua vumbi mjini Unguja huku kocha wa Simba akiwapa mbinu. Mechi hiyo inayotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa itafanyika kwenye Uwanja wa Amaan mjini Unguja.


Hata hivyo, Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Simba, Mcameroon, Joseph Omog ambaye hivi karibuni alifungashiwa virago na klabu hiyo, ameitaka Yanga kuhakikisha inacheza kwa nidhamu kubwa na URA kama inataka kuibuka na ushindi.

Akizungumza kwa njia ya simu kutoka kwao Cameroon, Omog alisema, kuwa wachezaji wa URA wanacheza kwa nidhamu kubwa na kwa ushirikiano wa hali ya juu ndiyo maana katika michuano hiyo timu hiyo inaonekana kuwa ni ngumu.

Alisema wachezaji wa Simba walipoteza umakini katika mechi zao na kushindwa kuzitumia vizuri nafasi walizokuwa wakizipata jambo ambalo ndilo limesababisha washindwe kuibuka na ushindi katika michezo yake. Amesema kwenye mechi dhidi ya URA walipoteza umakini ndiyo maana walifungwa kirahisi.

“Nimesikitishwa na kitendo cha Simba kuondolewa katika michuano hiyo lakini kila mtu anapaswa kukubaliana na matokeo hayo na hivyo ndivyo mchezo wa soka ulivyo. “Wachezaji wa Simba walipoteza kidogo umakini katika mechi hiyo ambayo video yake nimeiona leo (jana) kupitia mtandao baada ya kutumiwa na rafiki yangu mmoja ndiyo maana walifungwa japokuwa walicheza vizuri.

“Kwa hiyo, Yanga wanatakiwa nao kuwa makini katika mechi hiyo, kila mchezaji aingie uwanjani kupambana na kuyafanya majukumu yake kwa ufanisi mkubwa kama kweli wanataka kuibuka na ushindi, nimewaona URA ni wazuri na wanacheza kwa akili sana. “Yanga watafanya kosa kama watawaachia nafasi ya kutawala mchezo huo,” alisema Omog ambaye mwaka jana aliongoza timu hiyo kutinga fainali ya michuano hiyo lakini ikifungwa na Azam FC

Baada ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Lowassa kumtembelea Rais Magufuli...Mbowe azungumza haya

Baada ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa kumtembelea Rais John Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam na kufanya nae mazungumzo, Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe amesema kuwa kile kilichosemwa na Lowassa  sio msimamo wa CHADEMA bali ni mawazo yake binafsi.

Akizungumza jana na Idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji BBC, Mbowe alisema wao kama Chama wamekuwa na utaratibu wa kutoa msimamo wao na kueleza kuwa kwa siku za hivi karibuni wamekuwa na malalamiko dhidi ya Rais na Serikali yake kuhusu kuminywa kwa Uhuru wa Bunge, Mahakama na kuminya Demokrasia.

" Tunaona jinsi ambavyo uhuru wa watu unaminywa, uhuru wa vyombo vya habari, wandishi, wanasiasa na wananchi kutekwa, kudorora kwa uchumi, unaanzaje kumuunga mkono Rais nafikiri muhusika aulizwe mwenyewe," alisema Mbowe.

Kuhusu kauli ya Lowassa kusifia ongezeko la ajira, Mbowe anasema hayupo tayari kujibu hoja hiyo lakini akaeleza namna ambavyo makampuni mengi yanafungwa hivi sasa, kundi kubwa la vijana wasio na ajira likiwa mitaani.

" Nisikitike tu kuwa sisi tuna tatizo kubwa sana la kumuuguza Lissu ambaye alipigwa na risasi, kweli anaweza kutoka kiongozi mkubwa na kumsifia Magufuli wakati tunauguza watu? 

"Msaidizi wangu Ben Saanane amepotea hadi leo, wabunge wetu wanafukuzwa bungeni hivyo niseme tu hakuna msimamo kama huo ndani ya Chama labda atafutwe muhusika mwenyewe aeleze," Alisema Mbowe.

Akizungumzia hama hama kwa wabunge na wanachama wa upinzani na kujiunga na CCM sambamba na tukio la jana  la Mjumbe wa Kamati kuu ya Chama hicho, Muslim Hassanal kujiunga na CCM , Mbowe alisema suala la wapinzani kuhamia CCM halijaanza leo na kwamba suala la kujenga upinzani ulio imara lazima lipitie hatua mbalimbali ili kufanya mchujo wa kubakia na watu wenye dhamira ya kweli

Wanawake wenye ulemavu wa ngozi kuandika historia mpya kwa kupanda mlima Kilimanjaro.   Mwanaharakati wa haki za binadamu na mp...