Ijumaa, Agosti 25, 2017

TAARIFA MUHIMU KWA WATU WOTE WALIOOMBA NA WATAKAOOMBA KAZI SERIKALINI.



Mtakumbuka Serikali katika mwaka wa fedha uliomalizika 2016/2017 iliahidi kutoa Ajira serikalini zaidi ya 52,000 kwa Watanzania, ambapo katika siku za hivi karibuni Serikali imekuwa ikitoa vibali vya kuajiriwa watumishi wa kada mbalimbali ikiwemo Waalimu wa Sayansi, Kada za Afya na maeneo mengine kulingana na mahitaji.

Kama mnavyofahamu mojawapo ya jukumu la msingi la kuanzishwa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni pamoja na kuendesha mchakato wa ajira kwa niaba ya waajiri mbalimbali na hatimae kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi wanaofaulu usaili, ambapo tangu Serikali ilipoanza kutoa vibali baada ya kusitishwa tumeshapokea jumla ya vibali kwa ajili ya mamlaka za Ajira 239, kati ya hivyo vipo ambavyo vimeshafanyiwa kazi na vingine mchakato wake unaendelea katika hatua mbalimbali.

Aidha, baadhi ya vibali ambavyo mchakato wake umeshakamilika ni pamoja na  kibali cha Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ambayo tulipokea jumla ya  maombi ya kazi 6,852 na walioitwa kwenye usaili kutokana na kukidhi vigezo  walikuwa  2,949, kwa upande wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) maombi yaliyopokelewa ni  9,022 na walioitwa kwenye  usaili ni  1,550

Aidha, miongoni mwa taasisi ambazo mchakato wake bado unaendelea ni pamoja na Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili  (MUHAS) ambapo jumla ya maombi ya kazi 2,273 yamepokelewa na waliokidhi vigezo vya kuitwa kwenye usaili ni 144,  maombi yaliyopokelewa kwa ajili ya Wakala wa Serikali Mtandao (e-GA),yalikuwa 5,732 na  walioitwa kwenye usaili ni 4,054.  

Taasisi nyingine ambayo mchakato wake unaendelea ni pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambayo ina nafasi wazi za kazi 400 na jumla ya maombi ya kazi 56,815 yamepokelewa kupitia mfumo wa uwasilishaji wa maombi ya kazi kwa njia ya kielektroniki “Recruitment Portal’ na baada ya kufanyiwa kazi waliokidhi vigezo kwa mujibu wa sifa zilizokuwa zimeainishwa katika tangazo la kazi husika na kuitwa kwenye usaili ni 29,674.

Pamoja na nia ya Serikali ya awamu ya tano kuendelea kuhakikisha Watanzania wanaohitimu katika fani mbalimbali ndani na nje ya nchi wanapata kazi, zipo changamoto kadhaa ambazo zimekuwa zikijitokeza wakati wa utekelezaji wa mchakato wa ajira ambazo hupelekea baadhi ya waombaji kazi kutoitwa kwenye usaili. Kama mlivyoona katika takwimu zilizoainishwa hapo juu katika baadhi ya taasisi ambazo mchakato wake umeshafanyiwa kazi kupitia Sekretarieti ya Ajira.

Aidha, tungependa mzifahamu changamoto hizo ili mtusaidie kuendelea kuelimisha wadau wetu tukitambua mchango mkubwa wa vyombo vya habari katika kuelimisha na kuhabarisha jamii  ili nao waweze kuzifahamu, kuzielewa na kuzifanyia kazi ili nafasi nyingine za kazi zitapotangazwa waweze kuziepuka na kuwa katika nafasi nzuri na uhakika wa kuweza kuitwa kwenye usaili na hatimae kupata kazi wanazoomba.

Changamoto hizo ni pamoja na Waombaji wengi kutokufahamu namna ya kuandika barua za maombi ya kazi, kutoainisha nafasi wanazoomba, kutokusaini barua za maombi ya kazi wanazoziwasilisha, kutokuthibitisha nyaraka zao (certify) katika wanavyotakiwa kufanya hivyo, hususan kwa waombaji waliosoma nje ya nchi kutowasilisha vyeti vyao vya elimu kwa ajili ya uthibitisho wa kutambulika elimu walizozipata katika mamlaka husika kama NECTA, NACTE na TCU kabla ya kuzituma Sekretarieti ya Ajira.

Sambamba na hizo, ni baadhi ya waombaji kutokuambatisha nyaraka za elimu hususani cheti cha kidato cha nne na sita au astashahada, stashahada, shahada, shahada ya uzamili na kuendelea kulingana na elimu waliyonayo. 

Baadhi yao kutozingatia vigezo vya nafasi iliyotangazwa, ikiwemo kudanganya sifa wakidai wamemaliza shahada ya fani fulani ilihali hawajasoma shahada ya aina hiyo, au mwombaji mwenye elimu ya astashahada kuomba kazi ya shahada, kuandika barua moja ya kuombea kazi kwa nafasi tofauti, kutojua namna ya kuandika wasifu binafsi  (CV), waombaji wengi kuandika wadhamini wachache ambao ni ndugu zao badala ya idadi ya wadhamini inayotakiwa ambao wanauwezo wa kutoa taarifa zao za kitaaluma na kikazi kwa uhuru pindi wanapotakiwa kufanya hivyo.

Changamoto nyingine ni baadhi ya waombaji kazi wanapoelekezwa kuwasilisha picha za utambulisho wao “Pasportsize” wao wanapakia kwenye mfumo picha tofauti bila kujali mavazi wanayovaa, mandhari iliyotumika na aina za picha wanazotuma. 

Changamoto nyingine ni ya baadhi ya waombaji kazi ambao ni Waajiriwa katika Utumishi wa Umma kutokupitisha barua za maombi yao kwa Waajiri wao kabla ya kuziwasilisha Sekretarieti ya Ajira, pamoja na baadhi ya waombaji kuja kwenye usaili wa mchujo au mahojiano bila ya vyeti vyao halisi kama inavyoelekezwa.

Nyingine ni  waombaji wengi kutozingatia masharti ya jumla ikiwemo, kuwasilisha nyaraka pungufu mfano kutokuwasilisha barua ya maombi ya kazi, kutokuambatisha baadhi ya vyeti vya taaluma, kuwasilisha maombi, kwa njia tofauti na ile iliyoelekezwa kwenye tangazo la kazi,  kuwasilisha taarifa za uongo mfano, wasifu binafsi usio wa ukweli, kutopakia taarifa sahihi (upload) katika maeneo husika ya mfumo wa kuombea kazi pamoja na kupakia vyeti visivyokamilika mfano “result slips, partial transcript, provisional result, progress report, statement of result”.
Tumeainisha baadhi ya mapungufu hayo hapo juu ili wahitimu ambao ni waajiriwa watarajiwa wafahamu hivi sasa soko la ajira ni la ushindani mkubwa na linahitaji mwombaji aliyejiandaa vizuri. 

Tunaamini endapo muombaji yeyote wa kazi mwenye sifa na ambaye anazingatia maelekezo yanayotolewa na Serikali kwenye maombi ya kazi anayowasilisha ataitwa kwenye usaili. Kwakuwa wale ambao wahazingatii kikamilifu mara nyingi hukosa fursa ya kuitwa katika usaili na kuikosa nafasi anayotarajia na hatimae  kusababisha malalamiko.
Aidha, ni vizuri wakafahamu Serikali inatumia gharama kubwa katika kuendesha mchakato wa Ajira hadi kukamilika, na ni nia ya Serikali kuona kila nafasi inayotangazwa inapata mwombaji makini mwenye sifa, ujuzi na weledi wa kutosha kuweza kutumikia Taifa lake. 

Mwisho, nimalizie kwa kutoa rai kwa waombaji kazi wote wanaomba kazi serikalini kujiandaa kikamilifu pamoja na kuzingatia masharti ya matangazo husika kwa kuhakikisha wanaambatanisha nyaraka zinazotakiwa na kuomba nafasi za kazi ambazo wana sifa stahiki. 

Niwaahidi kuwa Sekretarieti ya Ajira itaendelea kutoa elimu zaidi na kuwataka wale wenye changamoto ambazo wanaona wanahitaji msaada wasisite kuwasiliana na taasisi kwa kufika katika Ofisi za Sekretarieti ya Ajira au kupitia mawasiliano yetu katika mitandao ya kijamii kama facebook.com/sekretarietiajira, twitter.com/psrsajira, instagram:psrsajira au kwa simu za kiganjani kupitia namba 0784398259/0687624975.
Imetolewa na; Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, tarehe 24 AGOSTI, 2017.

MAKONDA 'KERO YA KUKOSEKANA KWA MAJI JIJI LA DAR ES SALAAM SASA KWISHA KABISAA!!!'

Meneja uendeshaji wa mradi Mhandisi Lydia Ndibaleme akimuonesha Mkuu wa Mkoa Paul Makonda mchoro wa ramani wa mradi huo utakao jengwa katika eneo la Jangwani Jijini Dar es salaam

SERIKALI mkoani Dar es Salaam, imetangaza kujenga miradi  mitatu mikubwa   ya maji  itayo maliza tatizo la uhaba wa maji jijini humo.

MKUU wa Mkoa wa  Dar es Salaam, Paul Maonda,  ametembelea  miradi  mbalimbali  inayosimamiwa na Mamlaka  la Maji safi na Majitaka  mkoani Dar es Salaam (DAWASA).

Miradi hiyo ni  pamoja na ile ya uondoaji  na usafishaji wa majitaka, miradi wa uboreshaji  huduma za usambazaji  maji katika  baadhi ya maeneo  ya Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam.

Pia miradi ya uchimbaji wa  visima  katika wilaya ya Ubungo.

Lengo la ziara hiyo ilikuwa  kukagua maendeleo ya shuughuli mbalimbali za ujenzi wa miradi  mipya iliyo na lengo la  kumaliza tatizo la majisafi  na maji taka katika  jiiji la Dar es Slaam.

Huu ni muendelezo wa ziara zake alizo  anza hivi karibuni  ambapo tayari ametembelea chanzo kipya cha maji Kimbiji wilayani Kigamboni  ambako kuna miradi ya uchimbaji  wa visima virefu vyenye urefu wa kina cha mita 600 na miradi iliyokamilika  ya upanuzi  wa mitambo ya   Ruvu Juu na Chini mkoani Pwani.

Mradi wa ujenzi wa mitambo mitatu mikubwa  na ya kisasa ya kusafisha majitaka itakayo kwenda sabamba na ulazaji maboomba ya ukusanyji  maji taka itajengwa katika eneo la Jangwani, Mbezi beach  na Kurasini ili kuongeza kiwango cha` kusafisha  majitaa  cha asilimia 10  cha sasa kufikiaa asilimia 30 ifikapo mwaa 2020.
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa mradi tenki la maji eneo la Mabwepande Dsm
Gharma za  jumlaza miradi hii ni  dola milioni 600.

Miradi hii  inatekelezwa  kwa awamu tatu,  na awamu ya kwanza  inaanza ndani  ya mwaka huu wa fedha 2017/18.

Mradi wa mfumo wa majitaka  jangwani  unahusu  ujenzi wa mtambo wa kusafishia majitaka   ambapo ukapokamilika  utakuwa  n uwezo wa  kusfisha mta za ujazo 200,000 kwa siku.

Mfumo wa mabomba yenye  urefu wa kilomita 376 yatakay9lazwa kuanzia Ubungo hadi Jangwani, Kinondoni, Mwananyamala mdsasani  na katikati ya jiji utajengwa.
Afisa mtendaji mkuu wa Dawasco Cyprian Luhemeja (Kulia) akimuelezea Mkuu wa mkoa Paul Makonda namna mradi huo utakavyomaliza tattizo la maji Jijini Dar es salaam endapo utakamilika
Awamu ya kwanza ya ujenzi itahusisha sehemu  itakayoweza kusafisha mita  2500 kwa siku  na mabomba ya kilomit 17.43 yataakayojengwa katikaa eneo la magomeni.

Pia katika awamu ya kwanza  bomba linalomwaga majitakaa  baharini litaacha kutumika na badala yake majitaka hayo yatasafishwa  kwa kutumia mtambo huo.

Mtambo huo unajengwa kwa ushirikiano wa serikali ya Tanzania na  korea kupitia mkopo  wa  masharti nafuu  kutoka benki ya exim ya korea.

Unatarajiwa kugharimu  dola za marekani milioni 90. Taratibu  za ununuzi  zinaeendelea  ili  kumpata  mshauri  na hatimye mkandarasi  lengo likiwa ni kuanza ujenzi mapema mwaka 2018.
Mfumo  wa majitaka mbezi  utjengwa  kilongwima  na utakuwa na uwezo wa  wa ,kusafisha  mita za ujazo 16000 kwas iku . utajengwa na serikali ya Tanzania  kwa kushirikiana na  benki ya dunia kupitia mkopo  wa masharti nafuu na unatarajiwa kugharimu  dola milioni 65.

Ujenzi  wa mtambo wa kusafisha maajitaka kurasinini utakuwa na mfumo wenye urefu wa kilomita  90 utakaolazwa katia maeneo ya changombe , kurasini, temeke  na uwanja wa taifa.

Mradi huo utajengwa kwa kushirkiana  na  shirika la maendeleo la ufaransa  afd na utakuwa na uwezo wa kusafisha  mita za ujazo  11,0000 kwa siku.

Mitambo hiyo  itawezesha   kuzaisha gesi asilia  na umeme kwaajili ya kuendeshea  mkitambo  hiyo hivyo kupunguza  matumizi ya gharama za umeme na vilevile  maji yatakayokuwa  yametbiwa  yatauzwa  na kutumika katika shughuli mbalimbali  kama ile  kupoozea mitambo na umwagiliaji.

Tope litakaobakibaada ya mchkato huo  wa usafishaji majitaka  litaweza utmika kama mbolea  kwaajili ya  kilimo panja  na bustani za majani na miti ya kivuli na hivyo kupendezesha jiji.

Pamoja na miradi hiyo  mradi mwingine ni wa uboreshaji  mfumo wa usambazaji maji  ambao  unahusisha ujenzi wa matenki tisa ya kuhifadhia maji na kusambaza  maji yenhye ukubwa wa kuhifadhi  lita za ujazo milioni  tatu hadi milioni aita.

Meneja uendeshaji wa mradi Injinia Lydia Ndibaleme akizungumza na Waandishi wa habari katika ziara hiyo jinsi ambavyo wata utekeleza mradi huo namna ambavyo wananchi watanufaika kwa kiasi kubwa Pwani na Jijini Dar es salaam.

Pia ujenzi wa vituo  vine  vya kusukum maji, ununuzi  wa transifoma,  na ufungaji  njia za umeme   wa msongo wa  mkubwa   na ulazaji mabomba  makubwa  ya ugawaji  maji   na mabomba ya  usambazaji  maji yataayokuwa na urefu wa kilomomita 477.

Maeneo yanayotarajiwa kunufaika  na mradi huo  ni changanyikeni, bagamoyo,mpiji, zinga , kiromo , kitopeni  ukumi kerege buma mataya na ukanda maalumu ya eoz 

Lengo la mradi huu ni kuhakikisha wananchi wote  wa kawaida  wenye viwanda  na bashara katika eneo  lote la mradi wanapat huduma bora za maji hasa baada ya maji kuongezeka  kufuatia kukamilika kwa kazi zaupanuzi wa mitamb ya maji ya ruvu juu na ruvu chini.

Mradi huo utgharimu  dola za marekani milioni32 kupitia mkopo wa masharti nafuu kutoka serikali ya inda.

Pia  mradi wa uchimbaji wa visima katika manispaa ya ubungo  ili kuwapunguza changamoto wakati miradi mikubwa ya usambazaji  maji ikisubiriwa kutekelezwa.

Mkataba ulisainiwa aprili  11,2017 na unatarajiwa  kuisha agosti 31, 2017  mbapo visima 10 viatarajiwa kkuchimbwa   ambapo utagharimu   shilingi milioni109.

Wanawake wenye ulemavu wa ngozi kuandika historia mpya kwa kupanda mlima Kilimanjaro.   Mwanaharakati wa haki za binadamu na mp...