Alhamisi, Agosti 24, 2017


DC MJEMA 'Wanawake jitokezeni kwa wingi Jumamosi tujumuike sote na makamu wa Rais kwa ajili ya Uzinduzi wa jukwaa letu litakalotukomboa kiuchum'



 Mkuu wa wilaya ya ilala Bi sophia Mjema akizungumza na waandishi wa habari Hawapo kwenye picha siku ya leo kutoa taarifa rasmi za ufunguzi wa jukwaa la uwezeshwaji kiuchumi kwa wanawake



Katibu Mtendaji wa baraza la uwezeshaji kitaifa (NEEC)Beng' Issa akizungumza  na waandishi wa habari  siku ya leo katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya ilala kwa ajili ya kuzungumzia katika uzinduzi wa jukwaa la kina mama la uwezeshwaji kiuchumi litakalofanyika siku ya jumamosi


Baadhi ya wanahabari wakiendelea na majukumu yao ya kuchukua taarifa katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya ilala siku ya leo


Na Michael Utouh 

Makamu wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania siku ya jumamosi anatarajiwa kuzindua Jukwaa la uwezeshwaji kiuchumi kwa wanawake mkoa wa dar es salaam , jukwaa ambalo limelenga kwa ajili ya kumtoa mwanamke katika hali moja ya kiuchumi hadi hali nyingine ambapo takribani zaidi ya wanawake elfu tatu 3000 kutoka wilaya zote jijini Dar wanatarajiwa kushiriki zoezi hilo la uzinduzi.

Akizungumza na vyombo vya habari Mapema hivi leo Dc mjema amesema kuwa  Mgeni rasmi kwa ajili ya uzinduzi wa jukwaa la uwezeshwaji wanawake kiuchumi atakuwa ni Makamu wa Rais mheshimiwa Samia suluhu Hassan tukio ambalo litafanyika siku ya jumamosi ya tarehe 26/08/2017 kuanzia majira ya saa tatu kamili asubuhi huku akitaja eneo husika litakalo fanyika tukio hilo kua ni katika viwanja vya Posta kijitonyama kama unaelekea makumbusho ukiwa umetokea mjini posta barabara ya Bagamoyo

Akifafanua zaidi juu ya uzinduzi wa Jukwaa hilo la uwezeshaji wanawake kiuchumi ameongeza kwa kusema kuwa Makamu wa rais ndie aliezindua jukwaa hilo kwa mara ya kwanza na alilizindulia katika mkoa wa Dar es salaam na baadae akatoa maagizo kwa jukwaa hilo kuanzishwa na kuboreshwa kwa ngazi za kila Mikoa,Wilaya,tarafa,kata hadi mtaa na ndio maana siku ya jumamosi makamo wa raisi atazindua tena Jukwaa hilo la wanawake kiuwezeshaji uchumi kwa ngazi ya mkoa mzima wa Dar es salaam huku akitaja mkoa huo kuwa ni wa 23 katika uzinduzi wa jukwaa hilo tangu agizo hilo lilipotolewa rasmi.

'Napenda kutoa wito kwa wanawake pamoja kina mama wote kujitokeza kwa wingi ndio maana nasema Wanawake jitokezeni kwa wingi Jumamosi tujumuike sote na makamu wa rais kwa ajili ya Uzinduzi wa jukwaa letu litakalotukomboa kiuchumi.' Alisema mkuu wa wilaya

Naye Katibu Mtendaji baraza la uwezeshwaji kitaifa Beng'  IssaAmesema kuwa lengo la kuanzishwa kwa jukwaa hilo ni katika kuwaunganisha akina mama katika kuwasidia kupata mitaji,mikopo,mafunzo nk

Hivyo ametoa wito kwa akina mama wote wa mkoa wa Dar es salaam kujitokeza kwa wingi siku hiyo ya uzinduzi wa jukwaa la uwezeshwaji wanawake hasa akina mama wote wale wa kipato cha chini cha kati,na cha juu kuanzia akina mama ntilie hadi wote wafanyabiashara wakubwa kwa wadogo kusudi kupata kutambua mambo mengi yatakayo wasaidia kutambua pamoja na kukuzwa kifikra na uchumi pia .


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Wanawake wenye ulemavu wa ngozi kuandika historia mpya kwa kupanda mlima Kilimanjaro.   Mwanaharakati wa haki za binadamu na mp...