Ijumaa, Agosti 25, 2017

LHRC YALAANI VITENDO VYA UKIUKWAJI WA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU HAPA NCHINI

Mkurugenzi wa kituo cha haki za binadamu Helleni Kijo-Bisimba(kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo.

Na Anna Chiganga Utouh news,

Kituo cha Sheria na haki za Binadamu (LHRC) kimelaani vikali vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu vinavyoendelea nchini.ikiwa ni pamoja na  kitendo cha Wakala wa barabara nchini (Tanroads) kuidharau mahakama,na kuminywa kwa haki za wanasiasa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho, Hellen Kijo-Bisimba amesema wameshangazwa na uamuzi wa Tanroads wa kubomoa nyumba za wananchi wa Kimara hadi Kiluvya wakati wanapingamizi la Mahakama.

"Tunalaani kitendo hiki na tunashangazwa na uamuzi wa wakala wa barabara nchini Tanroads mkoa wa dar es salaam kuidharau Mahakama ambapo kwa lugha ya kisheria tunaita Contempt of Court amri iliyotolewa na mahakama kuu iliyoweka zuio LA kubomolewa nyumba za maeneo ya kimara hadi kibamba (kuiingilia Mahakama) "Amesema Kijo-Bisima.
Aidha ameongeza kuwa wanalaani kitendo cha kukamatwa ovyo kwa wanasiasa na kusema kitendo hicho ni kuminywa kwa haki za kisiasa na kiraia,ambapo viongozi wa vyama vya upinzani wanakamatwa ovyo ovyo bila kufuata misingi ya sheria na haki za binadamu.
"Hali hii imejitokeza sana kwa kuwanyanyasa wabunge wa vyama vya upinzani bila kufuata misingi ya kisheria na haki za binadamu katika ukamataji huo"Amesema
Pia amesema  ukamatwaji wa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na Mbunge wa Bunda mjini Ester Bulaya,aliyekamatwa akiwa hotelini kwa tuhuma za kutaka kuhudhuria mkutano nje ya jimbo lake na kudai kuwa huo ni ukiukwaji wa haki na kunyimwa uhuru wa vyama vya upinzani kufanya kazi yake.
Hata ovyo amesema kumekuwa na hali ya taaruki inayoendelea hapa nchini ya miili ya watu inayoelea kwenye Bahari ya Hindi ikiwa imefungwa kwenye viroba,ovyo wametoa with kwa serikali kufanya upelelezi wa tukio hilo ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.
Faceboo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Wanawake wenye ulemavu wa ngozi kuandika historia mpya kwa kupanda mlima Kilimanjaro.   Mwanaharakati wa haki za binadamu na mp...