Jumamosi, Oktoba 07, 2017

TANROADS YATANGAZA KUPUGUZA FOLENI JIJINI DAR.


JIJI la Dar es Salaam ni miongoni mwa miji inayokua kwa kasi barani Afrika na ukuaji wake kuathiri sekta mbali mbali za kijamii na kiuchumi hasa usafiri na usafirishaji.

Tangu miaka ya 1990 kumekuwa na mipango mbalimbali ya kuboresha usafiri Dar es Salaam ikiwamo kuanzisha barabara za aina mbalimbali, kama za mabasi yaendayo kasi, maegesho ya magari ya kulipia na kuhamasisha kujengwa kwa majengo yenye maegesho ya magari.

Pamoja na jitihada za serikali ya jiji na serikali kuu kuboresha usafiri bado kuna kero kubwa ya usafiri wa abiria, hasa wakati asubuhi na jioni hali inayowalazimu wananchi  kuchukua takribani saa tatu barabarani badala ya dakika 15 hadi 30 , kwa mfano, kutoka Mbezi ya Barabara Morogoro hadi katikati ya jiji na Kariakoo.

Ili kukabiliana na changamoto hiyo, tangu mwaka 2008 Wakala wa Barabara Nchini (Tanroads) Mkoa wa Dar es Salaam imetekeleza miradi maalum ya ujenzi wa barabara za kupunguza msongamano katika barabara kuu za jiji.

Mhindisi Miradi wa Ofisi ya Tanroads Mkoa wa Dar Es Salaam, Julius Ngusa, anasema mradi wa ujenzi wa barabara za pembezoni wa awamu ya tatu ni moja ya mikakati ya serikali ya kushughulikia tatizo sugu la msongamano wa magari ambapo utekelezaji wake ulianza tangu 2008/2009.

Anasema kupitia mradi huo, serikali ilichagua barabara tisa kwa ajili ya kujengwa katika viwango vya lami nazo ni barabara ya Ubungo (bus terminal)-Kigogo-Kawawa yenye kilometa 6.4, barabara ya Jet Corner-Vituka-Davis Corner urefu wa kilometa 12, nyingine ni Kinyerezi-Kifuru-Msigani-Mbezi Mwisho yenye kilometa 10.

Barabara ya Mbezi- Goba- Tangibovu yenye kilometa tisa, kadhalika ya Kimara Baruti-Msewe-Changanyikeni yenye urefu wa kilometa 2.6.

Ngusa, anazitaja barabara nyingine kuwa ni pamoja na Tegeta Kibaoni-Wazo Hill-Goba-Mbezi ndani ya Morogoro yenye kilometa 20, Kigogo Roundabout-Jangwani-Twiga katika bonde la Msimbazi ikiwa na kilometa 2.72.

Anazungumzia pia Tabata Dampo-Kigogo na Ubungo Maziwa- Mabibo External inayoingia Mandela inayojengwa kilometa 2.25 za lami.

“Miradi hiyo inajengwa katika awamu tatu za utekelezaji, ambapo hadi sasa awamu ya kwanza ya miradi hiyo iliyohusisha ujenzi wa barabara zenye jumla ya kilometa 19.42 tayari imekwishatekelezwa na kukamilika tangu 2008.”

Anaitaja miradi iliyokamilika kuwa ni pamoja na barabara ya Ubungo-Kigogo-Kawawa iliyokamilika mwaka 2010 kwa gharama ya Sh bilioni 11.44, Kigogo-Msimbazi-Jangwani iligharimu bilioni 7.64 ambayo ilikamilika mwaka 2017 pamoja na barabara ya Jet Corner-Vituka-Devis Corner iliyomalizika mwaka 2011.

“Kuhusu awamu  ya pili yenye urefu wa kilometa 27.5 na ujenzi wa daraja la Kinyerezi lenye urefu wa mita 40, kazi ilianza mwaka 2014 ambako hadi sasa zilizojengwa kwa kiwango cha lami ni pamoja na barabara ya Tangi Bovu (Samaki)-Goba iliyomalizika mwaka jana na kugharimu bilioni 8.6 ” anasema Ngusa.

Katika awamu hiyo mwaka 2016 serikali pia ilikamilisha ujenzi wa Barabara ya Tegeta Kibaoni-Wazo Hill-Goba-Mbezi Mwisho yenye kilometa 20, kwa gharama ya Sh bilioni 6.7.

Akifafanua zaidi Ngusa anasema miradi mingine iliyokamilika ni pamoja na Barabara ya Kilungule (Maji Chumvi)- External/Mandela yenye kilometa 3.3, ambapo mradi huo ulikamilika mwaka 2015 kwa gharama ya Sh. bilioni 4.4.

Aidha mradi wa barabara ya Kimara Baruti-Msewe wenye kilometa 2.6 uliopaswa kukamilika mwaka jana umeshindishwa kuisha kwa wakati kutokana na kutokuwepo kwa nafasi ya kujenga barabara, ambapo hata hivyo hadi kufikia 30 Septemba, 2017 mradi huo ulijengwa kwa asilimia 80.

Mhandisi Ngusa anasema awamu ya tatu ya utekelezaji wa miradi hiyo ulioanza mwaka 2016 na 2017 unahusika ujenzi wa barabara za Kifuru-Msigani, Goba-Makongo na Goba-Madale zenye urefu wa kilometa 14.1 na unatarajia kukamilika mwanzoni na nyingine mwishoni mwa mwaka 2018.

“Miradi ya barabara ya Goba-Madale na Goba-Makongo hadi kufikia Septemba 30, mwaka huu imekamilika kwa asilimia 52 wakati ule wa Kifuru-Msigani umefikia asilimia 87, malengo ni kuhakikisha kuwa miradi hii inamalizika kwa wakati kwa kuzingatia ubora na viwango tulivyojiwekea” anasema Ngusa.

Baadhi ya changamoto inayokabili miradi hiyo ni pamoja na wamiliki wa nyumba nyingi kuhitaji fidia, ambapo Tanroads kwa kushikiana na Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (Tarura) zimeanza uthamini na malipo yatalipwa na Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

Anasema serikali pia inaendelea na ujenzi wa barabara za Msongola-Mbande zenye kilometa moja nyingine ni Ununio-Mbweni urefu wa kilometa moja pia , Kitunde-Kivule yenye urefu wa kilometa 3.2, pia kilometa nyingine moja zinajengwa za barabara ya Dege-Gomvu.

Kukamilika kwa miradi hii kutaongeza tija na ufanisi katika kuchochea kasi ya maendeleo ya Dar es Salaam na taifa .

PSPF YAWAZAWADIA WAFANYAKAZI WAKE KWENYE KILELE CHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA DUNIANI

 NA KHALFAN SAID
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, amewapongeza wafanyakazi wa Mfuko huo, kwa kazi nzuri wanayofanya ya kuwatumikia wateja, (wanachama) wa Mfuko.
Bw. Mayingu ameyasema hayo wakati wa hafla fupi ya kuwatunuku tuzo na zawadi wafanyakazi waliofanya vizuri zaidi katika kipindi cha Wiki ya Huduma kwa Wateja, iliyoanza Oktoba 2 na kumalizika Oktoba 6, 2017.
Wiki hiyo ambayo huadhimishwa kila mwanzo wa wiki ya mwezi Oktoba kila mwaka, hulenga kuwakumbusha wafanyakazi wajibu wao wa kuwahudumia wateja kwa kuzingatia weledi wa utoaji huduma bora kwa mteja.
"Wakati nikiwa Iringa nimepokea pongezi nyingi za Wanachama wetu, wakiwapongeza nyinyi wafanyakazi kwa kuwahudumia vizuri, hongereni sana na niwaombe muendele kutoa huduma bora kwa wateja wetu kwani huo ndio wajibu wetu." Alisema Bw. Mayingu katika hafla hiyo iliyofanyika Oktoba 6, 2017 kwenye ukumbi wa makao makuu ya PSPF, Jubilee Tower jijini Dar es Salaam. 
Bw. Mayingu aliwapongeza wafanyakazi wa Mfuko huo kote nchini, kwa kazi nzuri na kuwaeleza kuwa kitendo cha wafanyakazi na maafisa wa Mfuko huo kutoka maofisini na kuwafata wateja, (wanachama) majumbani kwao ili kuzungumza nao na kuwahudumia kimesifiwa sana.
"Kaimu Mkurugenzi Mkuu, alifuatana na baadhi yenu kwenda kule Kipunguni B. na kukutana na mwanachama wetu, Bw. Kassim Mafanya, ambaye alikipongeza kitedo kile na kusema hakutegemea maishani mwake yeye kama mstaafu angetembelewa nyumbani kwake na PSPF, hili ni jambo jema." Alibainisha Bw. Mayingu.
Wafanyakazi waliopata tuzo ni Elizabeth Shayo, kutoka kitengo cha Huduma Kwa Wateja, Makao Makuu, ambaye kupitia teknolojia, (mifumo), ni wateja wenyewe ndio waliompendekeza kutokana na maoni yaliyopokelewa lakini idadi ya watu aliowahudumia.
Mwingine ni Bi.Valley Malinga, Afisa kitengo cha simu (Call Centre), ambaye naye alitunukiwa tuzo na kupewa zawadi kutokana na kuhudumia idadi kubwa ya wateja bila kuchoka.
Tuzo hizo pia zimekwenda kwa walezi wa mikoa wa PSPF, kampuni mshirika ya Ardhi Plan Limited na pia makampuni washirika yaliyoshirikiana na PSPF kwenye wiki ya huduma kwa wateja, ambayo ni pamoja na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, (NHIF), Mabenki ya CRDB, NMB, TPB na Mwalimu Commercial Bank (MCB).
 Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, akiwahutubia wafanyakazi na wadau wa Mfuko, wakati wa hafla ya kuwatunuku tuzo na kuwakabidhi zawadi wafanyakazi "waliochomoza" kwa utoaji huduma bora zaidi katika kipindi cha Wiki ya Huduma kwa Wateja, 2017, iliyofikia kilele Oktoba 6, 2017.
 Bw. Mayingu akimkabidhi tuzo, Elizabeth Shayo.
  Bw. Mayingu akimkabidhi tuzo, Bi.Valley Malinga
Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, (PSS), Bi. Mwanjaa Sembe, (wapili kushoto), akiwa na maafisa waandamizi wa Mfuko huo.
 Baadhi ya wafanyakzi wa PSPF
  Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, akiwahutubia wafanyakazi na wadau wa Mfuko, wakati wa hafla ya kuwatunuku tuzo na kuwakabidhi zawadi wafanyakazi "waliochomoza" kwa utoaji huduma bora zaidi katika kipindi cha Wiki ya Huduma kwa Wateja, 2017, iliyofikia kilele Oktoba 6, 2017.

Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bi. Neema Muro, akihutubia wakati wa hafla ya kuwatunuku wafanyakazi wa Mfuko huo mwshoni mwa Wiki ya Huduma kwa Wateja makao makuu ya Mfuko jijini Dar es Salaam Oktoba 6, 2017


Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bi. Neema Muro, akihutubia wakati wa hafla ya kuwatunuku wafanyakazi wa Mfuko huo mwshoni mwa Wiki ya Huduma kwa Wateja makao makuu ya Mfuko jijini Dar es Salaam Oktoba 6, 2017


Meneja wa Huduma kwa Wateja, Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bi. Laila Maghimbi, (kulia), na AfIsa Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. January Buretta, wakihakikisha kila kitu kinakuwa sawa kwenye hafla hiyo

Ijumaa, Oktoba 06, 2017

Magazeti ya leo Jumamosi September 7,2017

WASTAAFU WAIPONGEZA PSPF KWA KUPOKEA MALIPO YA PENSHENI YA MWEZI KWA WAKATI

 Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bi. Mwanjaa Sembe, (wapili kushoto), akimkabidhi kijarida cha Mfuko huo chenye maelezo ya shunguli mbalimbali zinazotekelezwa na PSPF, kwa Mwanachama wa Mfuko amabye ni Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), mstaafu, Mzee Thomas Martin  Kiama, (73), nyumabni kwake Oysterbay jijini Dar es Salaam wakati wa kilele cha Wiki ya Huduma kwa wateja leo Oktoba 6, 2017. Wengine pichani kutoka kushoto, ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi, na Afisa wa Unedeshaji Bw. Ernest Massay.


NA Khalfan Said

WANACHAMA wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, ambao ni wastaafu, wameupongeza Mfuko huo kwa kupata pensheni za kila mwezi kwa wakati.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara ya viongozi wa PSPF kutembelea Wanachama wake wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma Kwa Wateja Duniani, walisema kimsingi malipo ya pensheni ya kila mwezi yamekuwa yakiingia kwenye akaunti zao kwa wakati na bila usumbufu wowote.
“Mimi nashukuru penshni yangu napata bila shida, na inaingia kwenye akaunti yangu kwa wakati, hili napenda kuwapongeza sana.” Alisema Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (Mstaafu). Bw. Thomas Martin Kiama wakati alipotembelewa na ujumbe wa PSPF nyumbani kwake Oysterbay jana (Oktoba 6, 2017).
Najua zipo changamoto za hapa na pale, mimi ningependa muwe huru kabisa, ili muweze kutuhudumia vema sisi wanachama, vinginevyo huduma zenu nazifurahia, aliongeza Bw.Kiama, ambaye alistaafu mwaka 2005.
Kwa upende wake, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, nchini, Bibi. Mary Hariet Longway, naye aliipongeza PSPF kwa utoaji wa huduma na kwamba yeye anaridhishwa na utedaji kazi wake na kuwapongeza kwa kufika nyumbani kwake ili kupata maoni yake.
“Ninashukuru sana kwa kunitembelea kwani hii ni ishara ya jinsi mnavyotujali sisi wastaafu, lakini mimi kama Jaji mstaafu kwa utaratibu ulivyokuwa, sisi hatukuwa na bima za afya sasa kama mngetoa elimu ya jinsi ya kupata bima ya afya kupitia kwenu lingekuwa jambo jema.” Alishauri Bibi Longway amabye naye alistaafu mwaka 2005.
Alsiema, malipo ya kila mwezi ya Pensheni yake yamekuwa yakiingia kwenye akaunti yake bila shida yoyote.
Naye askari wa Jeshi la Magereza (mstaafu), Bw.Kasim Salehe Mafanya, yeye naye aliipongeza PSPF, kwa huduma bora lakini akaomba utaratibu ufanyike ili pensheni hiyo iweze kuboreshwa na hivyo kuelndelea kuwa na manufaa zaidi.
Akizungumza kwa niaba ya PSPF, Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, Bi. Mwanjaa Sembe, alisema, katika kuadhimisha Wiki ya Wateja Duniani, ofisi za PSPF kote nchini, zimefanya utaratibu wa kuwatembelea wanachama wake kwa lengo la kuwahakiki na kupokea maoni yao ili kuboresha utoaji wa huduma.
Aidha katika Ofisi za Makao Makuu, Wakurugenzi an Mameneja waliungana na maafusa na wafanyakazi wa Mfuko huo, katka kuwahudumia wateja waliofika makao makuu.

 Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa nchini, Bibi Mary Logway, ambaye  ni mwanachama wa PSPF, akizungumza nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam leo Oktoba 6, 2017, wakati alipotembelewa na Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa PSPF, Bi. Mwanjaa Sembe, kushoto.
 Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa PSPF, Bw. Gabriel Silayo, (wakwanza kushoto), akimsikilzia mteja (mwanachama) wa Mfuko, huku afisa aliye kwenye mafunzo kutoka Chuo Cha Usimamzi wa Fedha, (IFM), Bw. Paschal W. Divaz, (katikati), akifuatilia.
 Bw. Silayo akisalimiana na wateja (wanachama) waliofika makao makuu ya Mfuko kuhudumiwa.
 Mkurugenzi wa Uendeshaji wa PSPF, Bi. Neema Muro, (kulia), akimuhudumia mteja (mwanachama) aliyekifa makao Makuu kuhudumiwa.
Meneja wa Huduma kwa Wateja, PSPF, Bi. Laila Maghimbi, (kulia), na mteja wake, (mwanachama) wakifurahia jambo wakati mwanachama huyo akipatiwa huduma.
  Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa PSPF, Bw. Gabriel Silayo, wapili kulia), akizungumza na afisa aliye mafunzoni, kutoka chuo cha Usimamizi wa Fedha, 9IFM), Bw.Paschal W. Diaz
 Afisa Uchangiaji wa Hiari PSS, Bi.Mwajuma A.Mohammed, (kushoto), akimuhudumia mteja.
Afsia Mtekelezo, (CO), wa PSPF, Bi. Mwanaisha S. Waziri akiwa kazini.
 Afisa wa PSPF aliye mafunzoni, Bw. Alpha Mkopi, (katikati), akiwahudumia wateja, waliofika ofisi za Makao Makuu kupata huduma.
Maafisa wa PSPF wakitoa huduma Oktoba 6, 2017.
Mzee Kiama, (kushoto), akipitia maelezo ya uhakiki kabla ya kuweka saini yake. aliye nae ni Meneja wa Uchangiaji wa Hiari, (PSS), Bi. Mwanjaa Sembe.
 Mzee Kiama akiweka saini kwenye fomu ya uhakiki.
Bi. Mwanjaa Sembe, (kushoto), akimpa maelezo, Jaji Mstaafu, Bi. Mary Longway, kuhusu uhakiki wa uanachama wake PSPF.
Bi. Longway akiweka saini wkenye fomu hiyo ya uhakiki.
 Mkuu wa kitengo cha Mikopo kwa Wanachama wa PSPF, Bi. Linda Bahati, akizungumza na simu ya kikazi ili kupata maeelzo ya ziada wakati akimuhudumia mteja Oktoba 6, 2017.
 Afisa Uhsuiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi akizungumza na Mzee Kiama.
Jaji (mstaafu) Longway na mukuu wake, wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyaakzi wa PSPF waliomtembelea ofisini kwake Upanga jijini Dar es Salaam Oktoba 6, 2017.

Wanawake wenye ulemavu wa ngozi kuandika historia mpya kwa kupanda mlima Kilimanjaro.   Mwanaharakati wa haki za binadamu na mp...