MAMILIONI YA WAISLAMU DUNIANI WAKIOMBOLEZA SIKU YA ASHURA

Mamilioni ya Waislamu jana wameshiriki katika maombolezo ya kumbukumbu ya kuuawa shahidi Imam Hussein A.S katika siku ya Ashura.
Siku hii inajulikana kwa jina la Ashura ambapo katika siku hiyo Mjukuu wa Mtume (a.s.w.w) Imam Hussein bin Ali bin Abi Twalib alisimama kishujaa na wafuasi wake waaminifu 72 kukabiliana na jeshi kubwa la batili ili kulinda dini ya Allah.
katika kuikumbuka siku hiyo waislamu Duniani kote huomboleza katika siku 12 za mwezi wa Muharramu ambapo siku ya 9 katika siku hizo ndipo Imam Hussein (a.s) alipouawa na kilele chake huwa siku ya 10 ambayo ndio siku ya maombolezo yaani siku ya Ashura.
Lengo la Imam Hussein kuanzisha mapambano hayo ilikuwa ni kuamrisha mema na kukataza maovu pamoja na kuhusisha mafundisho na thamani ya dini ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w)
Karbala , Iraq katika siku ya Maombelezo, siku ya Ashura

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni