Jumapili, Oktoba 01, 2017

TAKRIBANI WAZEE 2530 WAPATIWA VITAMBULISHO VYA MATIBABU BURE WILAYA YA KINONDONI

Wazee waliofika katika halmashauri ya kinondoni jijini dar es salaam, na kuweza kuapatiwa vitambulisho vya matibabu bure.
 Mstahiki meya wa halmashauri manispaa ya kinondoni akizungumza na wazee waliofika katika maadhimisho ya siku ya wazee duniani na kuweza kupatiwa vitambulisho vya matibabu bure.


 Mstahiki meya wa manispaa ya kinondoni akigawa vitambulisho kwa wazee hao waliofika halmashaurini hapo.
Mzee Nassoro Juma akisoma risala kwa niaba ya wazee kata za halmashauri ya kinondoni jijini dar es salaam.

Ikiwa  leo Oktoba 1, 2017 siku ya wazee duniani Halmshauri ya Manispaa ya Kinondoni imewapatia vitambulisho vya matibabu bure Wazee 2530, sawa na asilimia 60 ya wazee 4166 waliotambuliwa huku kati yao Wanawake wakiwa 1838, Wanaume 2328.

Akizungumza katika maadhimisho hayo Mstahiki meya wa manispaa ya Kinondoni Benjamin Sitta ameeleza kuwa licha ya kuwapatia vitambulisho hivyo, amesema imewekwa mikakati maalumu ya kutambua changamoto nyingine za wazee ili waweze kuwawezesha wazee hao, ambapo pia amewashuri wajiunge katika vikundi ili iwe rahisi kuwafikia

Akisoma risala hiyo kwaniaba ya Wazee kata za Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Nassoro Juma Mataula wameishukuru serikali kwa hatua hiyo ya kuwapatia kadi za matibabu kwakuwa wamekuwa wakisumbuliwa na magonjwa mbalimbali na wengine hadi kupoteza maisha

Aidha wazee hao wameiomba Serikali kuwapa kibali kitakachowawezesha kusafiri bure au kufutiwa nauli za mabasi ya mwendo kasi, Mabasi yaendayo mikokani sambamba kuongezewa pensheni.

Kwa upande wake Mganga mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Festo John Dugange amesema zoezi hilo ni endelevu ambapo amewaomba wazee wajitokeze kwa wingi katika Ofisi ya Halmashauri au ofisi za kata zao ili kutambuliwa na kupewa vitambulisho vya matibabu bila malipo.

Maadhimisho ya sikuu hii katika wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es salaam yamefanyika Mwananyamala katika kata ya mkumbusho, na kitaifa yamefanyika Katika mkoa wa Dodoma.
Facebook

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Wanawake wenye ulemavu wa ngozi kuandika historia mpya kwa kupanda mlima Kilimanjaro.   Mwanaharakati wa haki za binadamu na mp...