Ijumaa, Machi 02, 2018

Wanawake wenye ulemavu wa ngozi kuandika historia mpya kwa kupanda mlima Kilimanjaro.

 
Mwanaharakati wa haki za binadamu na mpigania mabadiliko Jane Waithera akishirikiana Na mshindi wa tuzo ya muandaaji wa filamu na mpandaji wa milima mbalimbali Elia Saikaly wameandaa mradi unaojulikana kama "climb for Albinism"(kwea kwa ajili ya ualbino) ambapo wanawake sita kutoka Afrika wamejipanga kukwea mlima Kilimanjaro wenye kilele kirefu zaidi kuliko yote barani Afrika.

Akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam muanzilishi wa programu hiyo Elia Saikaly amesema kuwa Mara nyingi watu wenye ualbino wanaonekana kama waathirika na kusema kuwa wana mpango wa kuvunja dhana hiyo kwa kufanya kitu ambacho hakijawahi kufanyika na kusistiza kuwa wataionyesha dunia kwamba licha ya changamoto nyingi zinazowakabili na kusema kuwa wanawake hao wana nguvu, wana uwezo na ni mfano wa kuigwa kwa wanawake wengine duniani.

Aidha kiongozi mwenza wa "climb for albinism" Jane Waithera amesema kuwa watakaposimama kweye kilele cha Afrika, timu nzima itatuma ujumbe madhubuti utakaosaidia kuelimisha jamii na kuondoa mitizamo hasi inayoeneza fikra mbaya kuhusu watu wenye ualbino.

Kwa upande wake kiongozi wa shirika la under the same sun Peter Ash linalotetea haki na usitawi wa watu wenye ualbino kwa kuelimisha jamii kuhusu ualbino , amesema kuwa wanaunga mkono shughuli hizo za kupanda mlima huku akisisitiza kuwa wana ndoto kwamba siku moja watu wenye ualbino watachukua nafasi yao inayostahili kwenye jamii na kwamba siku za ubaguzi dhidi ya watu wenye albino zitakuwa kumbukumbu iliyofifia na kusema kuwa upandaji wa mlima huu utaionesha duniani kwamba ndoto hii inaweza kutimia.

Pia Nodumo Ncomanzi ambaye ni moja kati ya wapanda milima kutoka Zimbabwe amesema kuwa kupanda mlima ni njia nzuri itakayoonesha na kuwakumbusha watu kwamba albino Wapo na wanajitegemea na wanawake wenye ualbino wanastahili kupewa fursa ya kukabiliana na kuzishinda changamoto mbalimbali zinazowakabili.

RC MAKONDA AFANIKISHA NDOTO YA AHMED ALBAITY






Ndoto na shauku ya kijana Ahmed Albaity alieteseka kwa zaidi ya Miaka 10 Kitandani kwa kushindwa kumudu gharama za matibabu leo imebadilika kuwa furaha baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda kumkabidhi  Tiketi za Ndege za watu Wanne kwaajili ya safari ya kwenda kupatiwa matibabu Nchini China kwenye Hospital ya Beijing Puhua International huku akijitolea pia kugharamia fedha za Matibabu na Malazi.

 Makonda alitoa ahadi kumsaidia Ahmed Albaity wakati wa Zoezi la Upimaji Afya Bure kwenye Meli ya Jeshi la China mwishoni mwa Mwaka Jana baada ya kugundulika Ahmed anahitaji Matibabu Maalum ambayo hayapatikani kokote kule duniani isipokuwa China, jambo lililomfanya RC Makonda kutokwa na Machozi na Kuhaidi Kumpeleka kwenye matibabu kwa gharama yoyote ile *Maumivu na Mateso* anayopitia kijana huyo.

Ahmed Albaity anasumbuliwa na tatizo la uti wa mgongo baada ya kuanguka na kuvunjika Shingo alipokuwa akiogelea ambapo kwa sindano moja pekee inagharimu Dollars 26,000/= sawa na shillingi million 52.

RC Makonda amesema Ahmed atasafiri Nchini China Siku ya Jumapili akiongozana na watu watatu wa kumsaidia kumuhudumia ambapo gharama zake ni zaidi ya Shilingi Million 100.

Aidha RC Makonda amesema Shauku yake ni kugusa maisha ya Mwananchi hata kama ni mmoja atakaekwenda mbele za Mungu na kusema Asante Mungu kwa kutupatia viongozi wetu, ifike mahali tumtumikie Mungu katika nafasi zetu, na katika hilo watu wote watakuwa Sawa na tutawahudumia bila kutarajia chochote kutoka kwao kama sehemu ya utumishi wetu ambapo amewashukuru watu wote waliomchangia na kufanikisha matibabu.

Hata hivyo RC Makonda ametoa wito kwa wananchi wa dini zote kumuombea Ahmed ili aweze kupona na kuendelea na shughuli za ujenzi wa Taifa.

Kwa upande wa Ahmed Albaity amemshukuru RC Makonda kwa moyo wa ukarimu aliouonyesha ambapo ameeleza kuwa ameishi kwa mateso muda mrefu kutokana na kukosa uwezo wa kumudu gharama za matibabu.

Aidha amesema alipokuwa akiomba watu wamchangie wapo waliokuwa wakimvunja moyo kwa kumwambia hawezi kupona lakini RC Makonda ameonyesha moyo wa kipekee.

Wanawake wenye ulemavu wa ngozi kuandika historia mpya kwa kupanda mlima Kilimanjaro.   Mwanaharakati wa haki za binadamu na mp...