Ijumaa, Machi 02, 2018

Wanawake wenye ulemavu wa ngozi kuandika historia mpya kwa kupanda mlima Kilimanjaro.

 
Mwanaharakati wa haki za binadamu na mpigania mabadiliko Jane Waithera akishirikiana Na mshindi wa tuzo ya muandaaji wa filamu na mpandaji wa milima mbalimbali Elia Saikaly wameandaa mradi unaojulikana kama "climb for Albinism"(kwea kwa ajili ya ualbino) ambapo wanawake sita kutoka Afrika wamejipanga kukwea mlima Kilimanjaro wenye kilele kirefu zaidi kuliko yote barani Afrika.

Akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam muanzilishi wa programu hiyo Elia Saikaly amesema kuwa Mara nyingi watu wenye ualbino wanaonekana kama waathirika na kusema kuwa wana mpango wa kuvunja dhana hiyo kwa kufanya kitu ambacho hakijawahi kufanyika na kusistiza kuwa wataionyesha dunia kwamba licha ya changamoto nyingi zinazowakabili na kusema kuwa wanawake hao wana nguvu, wana uwezo na ni mfano wa kuigwa kwa wanawake wengine duniani.

Aidha kiongozi mwenza wa "climb for albinism" Jane Waithera amesema kuwa watakaposimama kweye kilele cha Afrika, timu nzima itatuma ujumbe madhubuti utakaosaidia kuelimisha jamii na kuondoa mitizamo hasi inayoeneza fikra mbaya kuhusu watu wenye ualbino.

Kwa upande wake kiongozi wa shirika la under the same sun Peter Ash linalotetea haki na usitawi wa watu wenye ualbino kwa kuelimisha jamii kuhusu ualbino , amesema kuwa wanaunga mkono shughuli hizo za kupanda mlima huku akisisitiza kuwa wana ndoto kwamba siku moja watu wenye ualbino watachukua nafasi yao inayostahili kwenye jamii na kwamba siku za ubaguzi dhidi ya watu wenye albino zitakuwa kumbukumbu iliyofifia na kusema kuwa upandaji wa mlima huu utaionesha duniani kwamba ndoto hii inaweza kutimia.

Pia Nodumo Ncomanzi ambaye ni moja kati ya wapanda milima kutoka Zimbabwe amesema kuwa kupanda mlima ni njia nzuri itakayoonesha na kuwakumbusha watu kwamba albino Wapo na wanajitegemea na wanawake wenye ualbino wanastahili kupewa fursa ya kukabiliana na kuzishinda changamoto mbalimbali zinazowakabili.

Maoni 1 :

Wanawake wenye ulemavu wa ngozi kuandika historia mpya kwa kupanda mlima Kilimanjaro.   Mwanaharakati wa haki za binadamu na mp...