Jumatano, Septemba 06, 2017

WANANCHI WAFURIKA KUPIMA AFYA BURE VIWANJA VYA MNAZI MMOJA

 wananchi waliofika katika viwanja vya mnazi mmoja kwa lengo la kupimwa afya zao wakipatiwa huduma.
 wananchi waliofika katika zoezi la upimaji wa afya viwanja vya  mnazimoja , litakalofanyika siku tano, kwanzia leo.

Zoezi la Upimaji wa Afya Bure kwa Muda wa Siku Tano limeanza leo kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja ambapo baadhi ya Wananchi wamewahi kwenye Viwanja hivyo tokea saa 10 Usiku.

Mwamko huu ni baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kutangaza zoezi la Upimaji bila Malipo.

Madaktari bingwa na Wauguzi kutoka Hospital za Umma,Jeshi na zile za Watu Binafsi wanaendelea na zoezi la Upimaji kwa Wananchi.

Katika Upimaji huo Mwananchi atakaepimwa na kubainika kuwa na matatizo ya kiafya atapelekwa Hospital na kupatiwa Matibabu Bure.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Wanawake wenye ulemavu wa ngozi kuandika historia mpya kwa kupanda mlima Kilimanjaro.   Mwanaharakati wa haki za binadamu na mp...