WATU 11 WASHIKILIWA NA POLISI KUTOKANA NA KUDHANIWA KUFANYA MAANDAMANO KUTOKANA NA TUKIO LA LISSU.
Watu 11 wakiwemo madiwani wanne wa Halmashauri ya Wilaya ya IKungi mkoani Singida wamekamatwa wakiwa na mabango yenye ujumbe wa kuishinikiza Serikali kutoa tamko kuhusu kuvamiwa na kupigwa risasi mwanasheria mkuu wa Chadema, Tundu Lissu.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Mtaturu amesema watu hao wamekamatwa na polisi jana Ijumaa mchana wakiwa na mabango katikati ya mji wa Ikungi, wakiwa kwenye harakati za kuhamasisha maandamano.
“Walitaka kufanya maandamano, tuliwawahi kabla hawajaanza, miongoni mwao wapo waliotokea Arusha na Dodoma, kwa hiyo wamekamatwa kwa ajili ya mahojiano zaidi," amesema Mtaturu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni