Jumatano, Septemba 06, 2017

WATU WANNE WA CHAMA CHA (CUF)WAFARIKI DUNIA KATIKA AJALI.

Wanne wa Chama cha Wananchi (CUF) wanaomuunga mkono mwenyekiti wa chama hicho anayetambulika na Msajili wa Vyama, Prof. Ibrahim Lipumba wamefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumatano September 6, 2017, baada ya msafara wao kupata ajali maeneo ya Ubenazomozi Mkoani  Pwani.

Ajali hiyo imetokea wakati viongozi hao wakitokea Dodoma kwenye sherehe za kuapishwa kwa Wabunge wapya wa Chama hicho baada ya gari lao kugongana na Lori.

Taarifa ya Mkurugenzi wa Habari wa CUF, Abdallah Kambaya viongozi waliofariki ni kutoka Wilaya ya Muheza, Tanga ambapo miongoni mwao ni Mgombea Udiwani wa Muheza Mjini, aliyefahmika kwa jina moja la Uredi.

Aidha, idadi ya majeruhi haijajulikana ila ni hawazidi 10 na baadhi yao wapo Hospital ya Tumbi huku akisema chanzo cha ajali hiyo ni gari la wafuasi hao kugongana na lori.
Facebook

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Wanawake wenye ulemavu wa ngozi kuandika historia mpya kwa kupanda mlima Kilimanjaro.   Mwanaharakati wa haki za binadamu na mp...